Nilivyofanikiwa Kupata Dream Job Baada ya Miaka Mitano ya Kuhangaika

Kwa miaka mitano mfululizo, maisha yangu yalikuwa kama mzaha wa hatima. Nilikuwa nimehitimu chuo kikuu nikiwa na matumaini makubwa, nikiamini nitapata kazi nzuri mara tu baada ya kupewa cheti. Lakini muda ulivyozidi kusonga, matumaini yale yalianza kufutika taratibu. Nilijaribu kila njia kutuma maombi, kuhudhuria usaili, hata kujitolea bila malipo lakini kila mara nilipata majibu yale yale: “Tutakujulisha.”

Nilianza kupoteza imani kabisa. Wakati wenzangu walikuwa wanapanda ngazi katika kazi zao, mimi nilibaki nikihangaika kutafuta hata nafasi ya mahojiano. Nilianza kufanya vibarua vidogo vya sokoni ili angalau nipate chakula cha siku. Mara nyingi nililala nikiwa na machozi, nikiwaza kwa nini maisha yalikuwa yamenigeuka namna ile.…CONTINUE READING